Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Tarehe 20 - 04 - 2025, kwa mara ya kwanza itafunguliwa Darul - Qur'an Jijini Mwanza - Tanzania kwa Jina la Imam Zainul - A'bidina (a.s). Sherehe ya ufunguzi wa Shule hiyo ya Qur'an Tukufu itafanyika katika viwanja vya shule hiyo inayopatikana katika katika maeneo ya ILOGANZALA, Mtaa wa Saba Saba. Hafla ya ufunguzi itaanza muda wa saa saba na nusu / 7:30 baada Sala ya Adhuhuri. Wageni mbalimbali wa Taasisi Mbalimbali za Kiislamu wamealikwa katika hafla hiyo, wakiwemo: Viongozi wa Serikali, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, na Bilal Muslim Mission of Tanzania.
17 Aprili 2025 - 18:47
News ID: 1550027
Your Comment